1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Kishida kuwatimua mawaziri wanaotuhumiwa kwa rushwa Japan

11 Desemba 2023

Vyombo vya habari nchini Japan vimeripoti leo kwamba waziri mkuu Fumio Kishida anatarajiwa kuwatimuwa mawaziri wake chungunzima wa ngazi za juu wanaochunguzwa kwa tuhuma za rushwa.

https://p.dw.com/p/4a21q
 Waziri Mkuu  wa Japan, Fumio Kishida.
Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida.Picha: Ezra Acayan/Reuters

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti maarufu nchini humo la Asahi Shimbun, jumla ya mawaziri 15 watatimuliwa ikiwemo manaibu mawaziri pamoja na viongozi wengine wa juu serikalini.

Ripoti zinaeleza miongoni mwa wanaokabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa wiki hii ni pamoja na Katibu mkuu Kiongozi  Hirokazu Matsuno ambaye ni msaidizi mkubwa wa waziri mkuu Kishida, pamoja na Yasutoshi Nishimura ambaye ni waziri wa uchumi viwanda na biashara.

Viongozi wote waliotajwa ni kutoka kambi ya waziri mkuu wa zamani Shinzo Abe, ambayo ni miongoni mwa kambi zinazowania ushawishi ndani ya chama tawala cha LDP.

Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba kambi hiyo ilishindwa kutowa taarifa juu ya maelfu ya dolla ilizopata kupitia uchangishaji.