1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Australia Kevin Ruud azuru Irak

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cf5t

Waziri mkuu mpya wa Australi, Kelvin Ruud, amefanya ziara ambayo haikutangazwa nchini Irak. Kiongozi huyo amekutana na waziri mkuu wa Irak, Nuri al Maliki mjini Baghdad.

Kwenye mkutano wa pamoja na wa waandishi wa habari, Kelvin Ruud ameahidi kwamba Australia itaendelea kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Irak na polisi wakati kikosi cha wanajeshi 550 kitakapoondoka nchini humo mwaka ujao. Australia ina wanajeshi takriban 1,500 nchini Irak.

Kelvin Ruud alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Australia mwezi uliopita na kumuondoa madarakani waziri mkuu John Howard, mshirika mkubwa wa rais George W Bush na aliyeunga mkono vita vya Irak vilivyoongozwa na Marekani.

Australia inapania kuwa muuzaji mkubwa wa ngano nchini Irak, mojawapo ya nchi inayoagiza zao hilo kwa wingi duniani. Mwaka jana Irak ilianza kununua ngano kwa wingi kutoka Marekani badala ya Australia.