1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri Mkuu wa Australia aahidi kushirikiana na China

Josephat Charo
6 Novemba 2023

Utawala wa Albanese umetafuta mahusiano ya maana na China huku ukikabiliana na ushawishi wa China unaokua katika eneo la Pasifiki.

https://p.dw.com/p/4YR1G
Australiens Premierminister Albanese besucht China
Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese akizungumza mjini Shangai 05.11.2023Picha: Lukas Coch/AA/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ameapa kushirikiana kwa makini na kwa njia nzuri na China huku nchi hizo mbili zikipania kuondosha misuguano katika mahusiano yao. Albanese alikuwa akizungumza jana Jumapili wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya biashara ya China mjini Shanghai, siku ya kwanza ya ziara yake ya kiserikali katika nchi hiyo ambayo ni mshirika mkubwa wa kibiashara.

Waziri mkuu huyo wa Australia anafanya ziara ya siku nne nchini China ambapo anatarajiwa kuugawa muda wake katika miji ya Shanghai na Beijing. Hii leo anatarajiwa kukutana na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing. Hii ni ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na waziri mkuu wa Australia nchini China katika kipindi cha miaka saba.

(afp)