1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu Sharon ziarani Ufaransa

Lillian Urio27 Julai 2005

Waziri mkuu wa Israe Ariel Sharon yuko ziarani nchini Ufaransa akiwa na lengo la kumaliza mvutano na tofauti kubwa zilizoko kati ya nchi hizo mbili. Ziara hiyo ya siku tatu inafanyika katika wakati ambao huko nyumbani wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiyahudi wakimlaani kwa mpango wake wa kuwaondoa walowezi kutoka kwenye maeneo ya Wapalestina.

https://p.dw.com/p/CHfi
Waziri Sharon akiwasili nchini Ufaransa kwa ziara ya siku tatu
Waziri Sharon akiwasili nchini Ufaransa kwa ziara ya siku tatuPicha: AP

Maafisa wa Ufaranasa wameielezea ziara ya Bw Sharon kuwa ni hatua mpaya , baada ya miaka kadhaa ya mivutano juu ya sera ya Ufaranasa kuelekea eneo la Mashariki ya kati na kuzidi kwa mashambulio dhidi ya jamii ya Kiyahudi nchini Ufaransa ambao ni jamii ya awachache yenye usahawishi ya kiasi ya awatu laki sita .

Balozi wa Israel mjini Paris, Nissim Zvili, alisema katika mahojiano kawmba ziara ya Waziri wake mkuu ni matukio ya kawaida ya juhudi za kurekebisha halui ya uhnusiano wa nchi zao zilizoanza mnamo miezi ya hivi karibuni.

Sambamba na ziara hiyo, waandamanaji kadhaa walikusanyika katikati ya jiji la Paris jana jioni wakipinga sera ya serikali ya Israel katika maeneo ya Wapalestina ya Gaza na ukingo wa magaharibi.

Nje ya kanisa la Madeleine linalokabiliana na bunge la Uafaransa, waandamanaji walionekana wakiwa na mabango yalioandikwa “Hapana kwa sera za Sharon”.

Waandamanaji walidai kuvunjwa kabiasa kwa ukuta unaojengwa kama uzio katika ukingo wa magharibi na mji wa Jerusalem, pamoja na kumalizwa mara moja hatua ya kuyakalia maeneo ya Wapalestina.

Maandamano hayo yaliandaliwa na jumla ya jumuiya na vyama vya kisiasa 50, ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya haki za binaadamu, ile inayopinga ubaguzi, Jumuiya ya mshikamano baina ya Ufaransa na umma wa wapalestina, chama cha kijani na chama cha kikoministi cha Ufaransa.

Mazungumzo ya Sharon na Viongozi wa Ufaransa yanakuja wiki tatu kabla ya Israel kuanza kuondoka kutoka ukanda wa gaza, jambo ambalo limetajwa na Rais wa Ufaransa Jacques Chirac kwamba ni la kijasiri.

Msaidizi wa Bw Sharon, alisema nchi yake ina hamu kubwa ya kupata uungaji mkono wa Ufaransa katika jitiahada za kusaka suluhisho la mzozo wa Israel na Wapalestina, ikiwa nchi hiyo itachukua msimamo usiopendelea upande wowote.

Uhusiano kati ya Israel na Ufaransa umekua wa matatizo kwa muda mrefu, kutokana na madai kwamba Ufaransa inawapendelea zaidi waarabu katika sera yake ya mashariki ya kati, bila kuzingatia wasi wasi wa Israel juu ya usalama wake.

Wakati huo huo huko Israel kwenyewe, vyombo vya habari vya Israel jana vilionyesha ibada iliyofanywa na wanaume 20 wa Kiisraeli, wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiyahudi, waliokusanyika kwenye kaburi la mtu aliyeishi enzi za kale, anayetukuzwa kwenye dini ya Kiyahudi, ili kumlaani waziri mkuu wa nchi hiyo.

Watu hao walifanya ibada inayoitwa Pulsa de Bura, maana yake kiboko cha moto, ina tokana na imani ya Kiyahudi ya Kabbalah. Matokeo ya ibada hiyo ni kifo kwa aliyelaaniwa katika kipindi cha siku 30.

Lakini kiongozi wa dini ya Kiyahudi Rabbi, Yohan Metzger, amesema anapinga Myahudi yoyote kufanya ibada kama hiyo, hata kama ibada hiyo sio ya kimsingi kwenye dini yao. Hawana haki ya kutumia dini kwa njia hiyo na hairuhusiwi kutumika dhidi ya Myahudi mwingine, hasa kama mtu huyo ni kiongozi wa Israel.