1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wazambia wanashiriki katika uchaguzi wa rais na Bunge

Saleh Mwanamilongo
12 Agosti 2021

 Wazambia wanapiga kura kwenye uchaguzi wa urais wakati nchi hiyo ikikumbwa na matatizo makubwa ya kiuchumi. Jumla ya wagombea 16 wanawania kiti cha urais.

https://p.dw.com/p/3ysf0
Raia wa Zambia wanaamua kati ya rais Edgar Lungu na mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema
Raia wa Zambia wanaamua kati ya rais Edgar Lungu na mpinzani wake mkuu, Hakainde HichilemaPicha: Patrick Mainhardt/AFP/Getty Images

Kura inafanyika wakati ambapo taifa hilo la Kusini mwa Afrika lenye utajiri wa shaba,linakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. Zoezi la upigaji kura lilianza mapema Alhamisi asubuhi kwenye zaidi ya vituo 12,000 baadhi vikiwa magerezani. Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, zaidi ya watu milioni saba sawa na asilimia 83 ya watu wenye umri wa kupiga kura walijiandikisha kwenye orodha ya uchaguzi.

Upinzani mkali unatarajiwa kuwepo kati ya wagombea wakuu wawili ambao ni rais wa sasa Edgar Lungu wa chama cha Patriotic Front (PF) na mgombea mkuu wa upinzani Hakainde Hichilema kutoka chama cha National Development (UPND).

Lungu atowa mwito wa utulivu

Rais Edgar Lungu ametowa ameomba kusiwe na visasi kwa watakao shinda
Rais Edgar Lungu ametowa ameomba kusiwe na visasi kwa watakao shindaPicha: Xinhua/imago images

Rais Edgar Lungu ambaye aliingia madarakani mwaka 2015,ni miongoni mwawaliopiga kura mapema leo  jijini Lusaka. Mara baada ya zoezi hilo, Lungu akielezea chama chake cha Patriotic Front ,alisema "Sisi ni timu iliyoshinda'', huku akiwahimiza watu kujitokeza kupiga kura.

''Maoni yangu ni kwamba Wazambia wako tayari kupiga kura na wamejitokeza kwa wingi, niliona foleni kadhaa nilipokuwa nikija hapa, hii inakumbusha kile kilichotokea mnamo mwaka 2011 wakati watu walipojitokeza kwa wingi na ninatumai kuwa watu wengi zaidi watakuja kupiga kura. Mgombea bora ashinde.", alisema Lungu.

''Uchaguzi unapaswa kuleta mabadiliko''

Mgombea wa upinzani na mfanyabiashara Hakainde Hichilema
Mgombea wa upinzani na mfanyabiashara Hakainde HichilemaPicha: Salim Dawood/AFP/Getty Images

Mpinzani wake mkuu ni Hakainde Hichilema mwenye umri wa miaka 59. Hii itakuwa mara ya sita kwa mpinzani huyo kuwania kiti cha urais katika nchi hiyo ya wakaazi milioni 18. Hichilema endepo atachaguliwa aliahidi kuwavutia wawekezaji na kusimamia vizuri uchumi wa Zambia kutokana na madai ya ufisadi.

Mfanyabiashara huyo aliwambia wandishi habari usiku wa kuamkia leo kwamba uchaguzi huo unapaswa kusababisha mabadiliko ya serikali.Vurugu ziliibuka wakati wa kampeni kati ya wafuasi wa chama cha PF cha Lungu na Chama cha Umoja na Maendeleo ya Kitaifa cha Hichilema. Matokeo rasmi yatatangazwa baada ya Jumamosi.

Zambia ilishuhudia ukuaji mkubwa wa uchumi muongo mmoja uliopita na hata ikaingia miongoni mwa mataifa ya uchumi wa kati lakini hivi sasa inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei, deni la taifa linaongezeka na madai ya rushwa iliyokithiri.