1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wawili washikiliwa kwa mauaji ya mwanariadha Kiplagat.

2 Januari 2024

Watu wawili watiwa mbaroni kwa kuhusishwa na tukio hilo mauaji ya mwanariadha wa Uganda, Benjamin Kiplagat, ambaye alipatikana akiwa amewuwa kwenye gari baada ya kuchomwa kisu nchini Kenya usiku wa kuamkia mwaka mpya.

https://p.dw.com/p/4amIh
Symbolbild I Polizei in Nairobi
Polisi wa Kenya, mjini Nairobi wakikabiliana na waandamani kutoka asasi za kiraia 03.04.2024Picha: Billy Mutai/SOPA/ZUMA/picture alliance

Kamanda wa polisi katika kaunti ndongo ya Moibe, Stephen Okal amesema kisu kinachoshukiwa kutumika katika mauaji ya mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 34 kilipatikana kwa mmoja wa washukiwa.Amesema nia ya mauji hayo yalitokea katika viunga vya mji wa Eldoret huko magharibi mwa Kenya yanadhamiwa kusukumwa na wizi kwa kuwa fedha na simu ya mkononi viliibwa.Kiplagat alishiriki katika michezo mitatu ya Olimpiki na michuano sita ya dunia katika mbio za mita 3,000. Alishinda medali ya shaba mwaka 2012 katika michuano ya Afrika.