1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kukutana juu ya mkataba wa kugawana wahamiaji

4 Oktoba 2023

Wawakilishi wa mataifa 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels kutafuta mwafaka ili kupata mkataba wa kugawana majukumu ya kuwashughulikia wakimbizi na wahamiaji wanaoingia Ulaya.

https://p.dw.com/p/4X6W4
Kundi la wahamiaji waliokolewa na madaktari wasiokuwa na mipaka katika bahari ya Mediterrania
Kundi la wahamiaji waliokolewa na madaktari wasiokuwa na mipaka katika bahari ya MediterraniaPicha: DARRIN ZAMMIT LUPI/REUTERS

Mkutano huo huo leo unafanyia kazi rasimu ya mkataba iliyopendekezwa na Uhispania iliyo mwenyekiti wa zamu wa mashauriano ya ndani ya Umoja wa Ulaya hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Hiyo itakuwa nafasi ya mwisho ya kufikia makubaliano kabla ya mkutano wa viongozi wakuu wa mataifa ya kanda hiyo utakaofanyika kuanzia kesho hadi Ijumaa huko Granada, Uhispania kujadili wimbi la uhamiaji barani Ulaya hususani wanaovuka kuptiia bahari ya Mediterrania.

Mvutano juu ya meli za hisani zinazowaokoa wahamiaji ulizuia kufikiwa kwa makubaliano wiki iliyopita lakini kuna matumaini suala hilo litatatuliwa kwenye mazungumzo ya hii leo.