1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroOman

Watu wanne wauawa kwa risasi karibu na msikiti Oman

16 Julai 2024

Watu wanne wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwa risasi karibu na msikiti mmoja huko Wadi al-Kabir mjini Muscat nchini Oman.

https://p.dw.com/p/4iM7w
Polisi ya Oman
Tukio hilo la ufyatuaji risasi ni tukio la nadra la usalama kutokea OmanPicha: AP/picture alliance

Hili ni tukio la nadra la uvunjifu wa usalama katika moja ya nchi zenye utulivu huko Mashariki ya Kati. Polisi wamesema hatua zote za usalama zimechukuliwa ili kuidhibiti hali hiyo, na kwamba uchunguzi umeanzishwa.

Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu Muscat umesema unafuatilia kwa karibu tukio hilo la ufyatuaji risasi na kuwataka raia wake kuwa makini na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka nchini humo.

Oman imedumisha sera yake ya kutoegemea upande wowote katika mizozo ya kanda hiyo na imekuwa ikijaribu kusuluhisha migogoro kadhaa ikiwa ni pamoja na ule kati ya Marekani na Iran.