1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu waliokufa kwa kimbunga Msumbiji yafikia 53

17 Machi 2022

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kimbunga Gombe kilicholikumba eneo la kaskazini mwa Msumbiji imefikia 53.

https://p.dw.com/p/48dRE
Mosambik | Schäden durch Tropensturm Gombe
Picha: Andre Catueira/EPA-EFE

Maafisa katika jimbo la Nampula wamesema idadi ya mwisho iliyotolewa ilikuwa watu 22, lakini miili mingine 31 imekutwa katika wilaya ya Mossuril.

Mety Gondola, afisa wa ngazi ya juu wa Nampula amesema jana usiku kuwa eneo hilo lililoko kwenye pwani ya Bahari ya Hindi, halifikiki kwa sasa kutokana na barabara kutatizwa na miti iliyoanguka.

Gondola amesema hali ni mbaya sana na idadi ya vifo inaweza ikawa ya juu zaidi, wakati wanaendelea na huduma za uokozi kwenye wilaya zilizoathirika zaidi.

Maelfu ya watu wameathiriwa na kimbunga Gombe katika jimbo la Nampula , ambalo lina watu wengi zaidi nchini Msumbiji.

Kimbunga hicho kilipiga Machi 11.