Kwa mara ya kwanza barani Afrika nchi ya Kenya itaandikisha historia kwa kuwapa nafasi watu walio na jinsia zote mbili kujitambulisha rasmi na kuhesabiwa kwenye sensa. Maandalizi ya sensa yanaelekea ukingoni na zimesalia kiasi ya wiki mbili kabla shughuli kuanza rasmi.