Watu sita wauawa Nigeria
27 Desemba 2016Matangazo
Mmoja wa wabunge wa zamani nchini humo, Gideon Morik, amethibitisha taarifa hizo hapo jana. Mapigano yaliyochukua muda mrefu kuwania ardhi na haki za maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo, yamesababisha vifo vya mamia ya watu katika maeneo ya katikati na kaskazini mwa Nigeria. Mbunge huyo alithibitisha kuuawa kwa watu hao sita akiwemo binti yake mwenye umri wa miaka 17, ambaye alikuwa amebakiza mwaka mmoja kabla ya kumaliza elimu yake ya sekondari. Aliongeza kuwa washambuliaji hao waliwajeruhi watu wengi na kuharibu nyumba kadhaa kabla ya kutoweka. Gavana wa jimbo hilo, Nasri El- Rufai, amelilaani shambulizi hilo.