1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Watu 60 wakamatwa baada ya uvamizi wa uwanja wa ndege Urusi

30 Oktoba 2023

Polisi ya Urusi imesema Jumatatu kuwa imewakamata watu 60 wanaoshukiwa kuuvamia uwanja wa ndege.

https://p.dw.com/p/4YBft
Machafuko hayo yameifanya Israel kuitaka Urusi iwalinde raia wake nayo Marekani ikalaani maandamano hayo iliyoyaita "maandamano ya chuki dhidi ya Wayahudi."
Machafuko hayo yameifanya Israel kuitaka Urusi iwalinde raia wake nayo Marekani ikalaani maandamano hayo iliyoyaita "maandamano ya chuki dhidi ya Wayahudi."Picha: AP/picture alliance

Uvamizi huo ulifanyika katika eneo lililo na idadi kubwa ya Waislamu la Dagestan, wakitaka kuwashambulia wayahudi wanaowasili kutoka Israel.

Kulingana na wizara ya usalama wa ndani ya Urusi maafisa 9 wa polisi walijeruhiwa walipokuwa katika harakati za kutuliza hali na wawili kati yao wamelazwa hospitalini.

Machafuko hayo yameifanya Israel kuitaka Urusi iwalinde raia wake nayo Marekani ikalaani maandamano hayo iliyoyaita "maandamano ya chuki dhidi ya Wayahudi."

Waandamanaji waliojitokeza, wengi walisikika wakisema "Allahu akbar" au Mungu ni mkuu, walivunja milango na vizuizi katika uwanja wa ndege wa Makhachkala Jumapili na wengine kuingia katika njia ya ndege.

Uwanja huo sasa uko chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya usalama.