1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 39 wauwawa Mashariki Congo

31 Mei 2021

Shirika moja linalofuatilia masuala ya usalama limesema leo karibu watu 39 wameuwawa katika mashambulizi mawili mapya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo

https://p.dw.com/p/3uDag
Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Shirika hilo la Kivu Security Tracker KST limesema takriban watu 20 wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Boga na wengine 19 katika kijiji cha Tchabi katika eneo la Irumu mkoani Ituri.

Kiongozi mmoja wa mashirika ya kiraia amelilaumu kundi la Allied Democratic Forces ADF kwa mauaji hayo.

soma zaidi:Waasi 10 wauwawa mashariki mwa Kongo

Likiwa ni kundi la Kiislamu kutoka Uganda kihistoria, ADF ambalo limesababisha umwagikaji mkubwa wa damu ni mojawapo ya makundi yaliyojihami ambayo yako mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Shirika la Kivu Security Tracker linasema ADF imewauwa zaidi ya watu 1,200 huko Beni pekee tangu mwaka 2017.