1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 38 wateketea kwa moto kwenye gereza kuu Burundi

Saleh Mwanamilongo
7 Desemba 2021

Moto mkubwa umelitekezeta gereza moja lenye msongamano wa watu nchini Burundi. Wafungwa wengine kadhaa wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/43wsO
Burundi | Straßenszene in Bujumbura
Picha: DW/A. Niragira

Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza, alityembelea eneo la msiba akiwa na mawaziri kadhaa, aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu 38 walikufa kwenye moto huo na wengine 69 wamejeruhiwa vibaya.

Moto huo ulizuka mwendo wa saa 10 alfajiri.Wizara ya mambo ya ndani ilisema kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa ulisabaishwa na hitilafu ya umeme.

Mfungwa mmoja ameliambia shirika la habari la AFP kuwa walipouona moto walianza kupiga kelele lakini polisi walikataa kufungua milango ya vyumba wakisema hayo ni maelekezo waliyopokea.

Msongamano wa wafungwa

Burndi Gitega Polizei

Wale waliokuwa na majeraha mabaya zaidi wamepelekwa hospitalini, wengine wakibebwa kwenye malori ya polisi, huku wengine waliokuwa na hali mbaya zaidi walitibiwa katika eneo la tukio, mashahidi walisema.

Jela hiyo yenye takriban miaka 100, ni ya tatu kwa ukubwa nchini Burundi, kulikuwa na zaidi ya wafungwa 1,500 hadi mwishoni mwa Novemba, kulingana na takwimu za mamlaka ya magereza, juu sana kuliko uwezo wake iliyoundwa wa 400.

 Vikosi vya shirika la Msalaba Mwekundu nchini Burundi vilikuwa katika eneo la tukio kuwahudumia waathiriwa, na moto huo sasa umedhibitiwa, walioshuhudia walisema.