1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 22 wafariki baada ya jengo la shule kuanguka Nigeria

13 Julai 2024

Karibu wanafunzi 22 wamekufa baada ya jengo la shule kuanguka wakati wa masomo huko nchini Nigeria. Hayo yamesemwa na mamlaka nchini humo.Wanafunzi wengine 130 wanapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwenye mkasa huo

https://p.dw.com/p/4iFbX
Nigeria |  Jos
Picha ikiwaonyesha watu wakiendelea na shughuli ya uokozi katika shule iliyopo katika mji wa Jos Nigeria baada ya jengo la shule kuangukaPicha: AP Photo/picture alliance

Karibu wanafunzi 22 wamekufa baada ya jengo la shule kuanguka wakati wa masomo huko nchini Nigeria. Hayo yamesemwa na mamlaka nchini humo.

Karibu wanafunzi wengine 130 wanapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwenye mkasa huo, ambapo wengi wa wahanga ni wanafunzi na watumishi wa shule.

Soma zaidi. Wanafunzi wafariki baada ya shule kuporomoka Nigeria

Afisa wa habari na mawasiliano wa jimbo la Plateau, Musa Ibrahim Ashoms amesema jengo hilo lilikuwa ni sehemu ya shule ya upili ya Saint Academy iliyoko katika mji wa Jos.

Idadi ya vifo inatajwa kuwa huenda ikaongezeka, kwa kuwa karibu wanafunzi 200 wanaaminiwa walikuwa kwenye jengo hilo. Shughuli ya uokozi inaendelea na tayari kumeanzishwa uchunguzi wa mkasa huo.