1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Watu 17 wauawa Goma na wengine 370 wamejeruhiwa

28 Januari 2025

Mapigano katika mji uliozingirwa wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha vifo vya takriban watu 17 na kuwajeruhi wengine 370.

https://p.dw.com/p/4pkDf
DR Kongo | Jeshi la serikali
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Wang Guansen/Xinhua/picture alliance

Jeshi la Kongo linaendelea kupambana na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda. Raia watano wameripotiwa kuuawa huko Gisenyi nchini Rwanda.

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa mzozo huo unaweza kuzusha vita vipana zaidi vya kikanda na ukaelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mbaya ya kibinadamu huko Goma ambako mwezi huu pekee, karibu watu 500,000 wameyahama makazi yao.

Soma pia:Waandamanaji washambulia balozi za kigeni Kinshasa

Rais wa Kenya William Ruto, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameitisha mkutano wa marais wa Jumuiya hiyo hapo kesho na wakati huohuo akizitaka Ufaransa na Marekani kuunga mkono juhudi za kikanda za kuutafutia suluhu mzozo huo wa mashariki mwa Kongo.