1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watayarishi michezo ya olimpiki Tokyo wahakikishiwa viwanja

Sekione Kitojo
12 Juni 2020

Watayarishaji wa michezo ya Olimpiki  ya Tokyo wamesema  wamepata ruhusa ya kutumia vingi ya viwanja ambavyo hapo kabla  vilipangwa kufanyika  michezo hiyo iliyoahirishwa hadi mwaka ujao .

https://p.dw.com/p/3dfxX
Toshiro Muto
Picha: AFP/STR/Jiji Press

Mkuu  wa  kamati ya matayarisho  ya  michezo  ya  olimpiki  mjini Tokyo Toshiro Muto  amesema  baada  ya  mkutano  wa  bodi  kuwa wamepata  uthibitisho kutoka kwa  asilimia  80 ya  wale wanaohusika na  viwanja  hivyo kuwa tunaweza  kuvitumia.

Amesema  mazungumzo  yanaendelea  na  viwanja  vingine , ikiwa  ni pamoja  na  kijiji  cha  olimpiki.

Japan Tokio Olympische Spiele verschoben
Mashindano ya olimpiki mwaka huu 2020 yalikuwa yafanyika mjini Tokyo lakini yameahirishwa kutokana na janga la virusi vya coronaPicha: AFP/C. Triballeau

Watayarishaji  nchini  Japan  wanataka  kufanya  michezo  hiyo  kwa njia  rahisi  kuliko  ilivyopangwa  hapo  kabla ili kuepuka gharama. Wakati  huo  huo afya  ya  wanamichezo , maafisa  na  watazamaji ni  muhimu  sana  kutokana  na  janga  la  virusi  vya  corona.