1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasociasl Democratic waingia madarakani Canberra

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CStp

Canberra:

Waziri mkuu mteule wa Australia Kevin Rudd wa kutoka chama cha Labour anasema atashiriki katika mkutano wa mwezi ujao wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa huko Bali Indonesia,ili kubainisha dhamiri zao za kujitenganisha na sera za mtangulizi wake John Howard.Mwanasiasa huyu wa kihafidhina aliyesimama bega kwa bega na rais George w. Bush kupinga itifaki ya Kyoto,amekiri serikali yake ya muungano imepoteza asili mia 6 ya kura.Matokeo ya hadi sasa yanaonyesha kwamba chama cha Labour kimejikingia viti 86 kati ya 150 vya bunge.Kevin Rudd anapanga kutangaza baraza lake la mawaziri wiki ijayo.Mataifa kadhaa shirika ya magharibi,ikiwemo Uengereza,nchi jirani za asia na baadhi ya makundi ya wakaazi asilia wa Australia-Aborigines,wamesifu kubadilika yerikali nchini Australia.Katika kampeni yake ya uchaguzi Kevin Rudd aliahidi pia kuwarejesha nyumbani wanajeshi 550 wa Australia kuitoka Iraq.