1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSlovakia

Raia wa Slovakia wapiga kura kumchagua rais

6 Aprili 2024

Raia nchini Slovakia wanapiga kura hii leo kumchagua rais mpya ambaye atakuwa pia na jukumu la uanachama katika Umoja wa Ulaya na pia kwenye Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4eV8z
Slovakia | Uchaguzi
Mwanamume akipiga kura kwa uchaguzi wa urais katika kituo cha kupigia kura huko Bratislava, Slovakia, Jumamosi, Aprili 6, 2024.Picha: Denes Erdos/AP/picture alliance

Ivan Korcok, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na muungaji mkono mkubwa wa Ukraine anachuana na Spika wa zamani Peter Pellegrini kuziba pengo la Rais Zuzana Caputova.

Wagombea hao wameingia kwenye duru muhimu ya pili baada ya kushindwa kufikia asilimia 50 ya kushinda moja kwa moja kwenye duru ya kwanza mwezi uliopita.

Ingawa cheo hicho si cha kiutendaji, lakini Rais wa Slovakia ndio huidhinisha mikataba ya kimataifa, kuteua majaji wakuu na kamanda mkuu wa majeshi, lakini pia anaweza kupiga kura ya turufu bungeni. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa usiku wa leo.