1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasichana kuvaa na kuwacha matiti wazi ni fasheni au uhuni?

19 Septemba 2012

Namna unavyovaa kuna maana kubwa na ndio maana mitindo ya mavazi ni moja ya masuala yanayopewa kipaumbele na vijana wengi, lakini baadhi ya wakati vipaumbele hivyo vinaweza kuzua mitizamo tofauti katika jamii.

https://p.dw.com/p/167oL
Wanamitindo wakivaa aina mbalimbali za Cleavage.
Wanamitindo wakivaa aina mbalimbali za Cleavage.Picha: picture-alliance/dpa

Katika makala hii ya Vijana Mchakamchaka, Stumai George anajadili kuhusu fasheni ya vijana wa kike kuvaa nguo inayoacha wazi sehemu ya matiti, au Cleavage kwa lugha ya Kimombo. Anazungumza na vijana wenyewe kujua sababu na hata mitazamo iliyopo juu ya vazi hilo. Je, ni vijana wote wa kike wanaovutiwa nalo? Je, vijana wa kiume wanafurahikiwa nalo?

Kusikiliza makala hii, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Stumai George
Mhariri: Othman Miraji