1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Rais Bush akutana na Sarkozy wa Ufaransa

12 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBa8

Rais wa Marekani George Bush alikutana na Rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy katika nyumba yake iliyo kwenye gfuo za bahari.Mkutano huo unalenga kuimarisha uhusiano kati ya Ufaransa na marekani hususan suala la uvamizi wa Iraq.Mkutano huo ni wa tatu kati ya viongozi hao wawili tangu Bwaana Sarkozy kuingia madarakani mwezi mei mwaka hu.

Masuala mengine waliojadilia ni mpango wa Nuklia wa Iran.

Wazazi wake Rais Bush…rais wa zamani George HW Bush na mkewe Barbara Bush walimlaki Rais Sarkozy.

Rais Bush alisisitiza kuwa mkutano huo haukuwa rasmi na ulilenga hasa mazungumzo ya kirafiki.

Rais Sarkoza kwa upande wake anaahidi ushirikiano zaidi na Marekani huku akiwa likizo katika mtaa ulio karibu na makao ya Rais Bush ya binafsi katika jimbo la New Hampshire.

Mtizamo wa Rais Sarkozy unatofautiana na ule wa rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac aliyekuwa na migongano na Rais Bush jambo lililomfanya kuhamasishaa jamii ya kimataifa kupinga uvamizi wa Iraq.