1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Shirika la fedha la kimataifa launga mkono amarekebisho.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Du

Shirika la fedha la kimataifa-IMF, limeunga mkono marekebisho yenye lengo la kuimarisha msimamo wa nchi zinazoendelea katika shirika hilo. Watungaji sera kutoka shirika hilo la fedha pia wameahidi kupunguza matumizi na kuimarisha uwajibikaji. Mkutano wa mwaka huu wa Shirika la fedha la kimataifa na Benki ya dunia umekuja wakati kukiwa na ukuaji wa taratibu wa uchumi duniani na kupanda kwa bei ya mafuta.