1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON. Sharon aahidi kuwaachilia wafungwa zaidi wa Palestina.

25 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAQ

Waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon, ameahidi kuwaachilia huru wafungwa 400 wa kipalestina kama ishara ya kumuunga mkono rais wa Palestina, Mahmoud Abbas.

Akiihutubia kamati inayohusika na maslahi ya wayahudi wa Marekani mjini Washington, Sharon ameahidi atashirikiana na viongozi wa Palestina katika mpango wake wa kuyaondoa makazi ya wayahudi kutoka mkanda wa Gaza.

Hapo awali serikali ya Sharon iliwaachilia wafungwa 500, ambao mamlaka ya Palestina inasema ni idadi ndogo kwa mujibu wa makubaliano yaliyoafikiwa huko Sharm el Sheikh nchini Misri. Matamshi hayo yametolewa kabla ya mkutano kati ya rais George W Bush na rais Mahamoud Abbas katika ikulu ya white house.