1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Sarkozy ziarani Marekani.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79J

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy yuko mjini Washington Marekani kwa ziara yake ya kwanza rasmi kukutana na mwenzake wa Marekani, george W. Bush. Mkutano huo unaonekana kuwa ishara ya mabadiliko ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili tangu pale rais Sarkozy alipoingia madarakani mapema mwaka huu.

Nchi hizo mbili zimezika tofauti zao wakati rais George W. Bush alipomlaki rais huyo wa Ufaransa katika Ikulu ya Marekani , na kuweka kando miaka kadha ya uhusiano usiokuwa mzuri kutokana na vita ya Iraq. Sarkozy ambaye amepata mapokezi ya zulia jekundu , amesema kuwa amekwenda Marekani kuziteka upya nyoyo za Wamarekani na wakati huu kwa muda mrefu zaidi. Mazungumzo yao yatalenga zaidi kuhusu hatua za kuleta amani katika mashariki , pamoja na mpango wa kinuklia wa Iran. Anatarajiwa kulihutubia baraza la Congress leo.