1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington/Ramallah: Marekani imekiri ufanisi haujafikiwa kama ilivyokua ikitarajiwa katika mzozo wa mashariki ya kati.

9 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkx
Waziri wa mambo ya nchi za nje Colin Powell amekiri hayo wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Washington.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ameuhimiza utawala wa ndani wa Palastina upambane kwa nguvu zaidi dhidi ya ugaidi na kuisihi Misri izidi kuwashinikiza wapalastina.Waziri Colin Powell anashikilia uwezekano wa kuundwa madola mawili kama njia ya kuufumbua mzozo wa mashariki ya kati.Amekosoa kitisho cha hivi karibuni kilichotolewa na waziri mkuu wa utawala wa ndani wa Palastina Ahmed Qorei.Bwana Qorei alisema pindi Israel ikiendelea kupanua mpaka wake katika maeneo ya ukingo wa magharibi,wapalastina wanaweza kuachilia mbali lengo la kuunda dola lao na badala yake kupigania taifa la wakaazi wa jamii mbili-waarabu na wayahudi.Hali hiyo itamaanisha wapalastina wataibuka kua jamii ya walio wengi katika taifa kama hilo.