1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Marekani na Ufaransa zimedhamiria kuimarisha uhusiano wao ...

16 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFik
uliodhoofika.Waziri wa ulinzi wa Ufaransa bibi Michele Alliot-Marie amesema baada ya mazungumzo pamoja na waziri mwenzake wa Marekani Donald Rumsfeld mjini Washington ,tunanukuu:"hali imeanza kuboreka".Kumekua na azma ya dhati ya kumaliza mvutano."Mwisho wa kumnukulu.Mazungumzo ya saa moja kati ya bwana Rumsfeld na waziri mwenzake wa Ufaransa Alliot-Marie yalikua ya kwanza ya daraja hiyo tangu vita vya Iraq viliporipuka.Ufaransa iliongoza kundi linalopinga vita vya Iraq,zikiwemo pia Rashia na Ujerumani.Wakati huo huo Mtawala wa Marekani mjini Baghdad Paul Bremer atawasili Washington baadae hii leo kwa mazungumzo pamoja na rais George W. Bush.Mazungumzo yao yatafanyika kabla ya bwana Paul Bremer kuhudhuria mkutano uliotishwa na Umoja wa mataifa kuhusu Iraq,jumatatu ijayo mjini New-York.