1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji wa kujitenga wamwua wafanya kazi Assam

22 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFyx
NEW DELHI: Nchini India wameuawa si chini ya watu wanane yalipotokea mapigano katika mkoa wa Assam. Watu waliouawa ni wafanya kazi kutoka mkoa jirani wa Bihar, viliripoti vyombo vya habari vya India. Polisi wamewashutumu wapigania wa kujitenga wa Mwungano wa Vyama vya Ukombozi kufanya kitendo hicho. Kwa sababu ya uhaba mkubwa wa nafasi za kazi mkoani Assam hivi karibuni limezuka wimbi kubwa la kuwapiga vita watu wanaokuja kutafuta kazi kutokea mikoa mengine.