1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapigajai jihadi 44 wapatikana wamekufa katika jela Chad

Sekione Kitojo
19 Aprili 2020

Kundi la washukiwa 44 wa kundi la Boko Haram,waliokamatwa katika operesheni ya hivi karibuni dhidi ya kundi hilo,wamepatikana  wamefariki katika chumba cha jela, huenda kwa sumu, mwendesha mashitaka mkuu wa Chad amesema.

https://p.dw.com/p/3b7qW
Symbolbilder Niger Armee
Wanajeshi wa Chad wakilinda doria dhidi ya kundi la Boko HaramPicha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Akizungumza  katika  televisheni  ya  taifa, Youssouf Tom  amesema wafungwa 44 walikutwa wamekufa katika  chuma  walimofungiwa siku  ya  Alhamis.

Uchunguzi  uliofanywa  kwa watu wanne  miongoni  mwa  waliofariki umeonesha aina  ya  kitu  hatari  ambacho  kimesababisha  matatizo ya  moyo katika  baadhi  ya  waliofariki  pamoja  na  matatizo makubwa ya  kupumua  kwa  wengine, amesema.

Nigeria | Niedergebrannte Fahrzeuge in Auno
Mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Boko Haram katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria Picha: Getty Images/AFP/A. Marte

Waliofariki walikuwa  miongoni mwa  kundi  la  washukiwa 55 waliokamatwa  katika  wakati  wa  operesheni  kubwa  ya  jeshi katika  eneo  la  ziwa  Chad iliyoanzishwa  na  rais Idriss Deby Itno mwishoni  mwa mwezi  Machi.

"Kufuatia  mapigano  katika  eneo  la  ziwa  Chad, wanachama 58 wa  kundi  la  Boko  Haram walikamatwa  na  kupelekwa  N'Djamena kwa ajili  ya  uchunguzi  zaidi,"  amesema  Tom.

"Siku  ya Alhamis  asubuhi, waliowafunga  walituambia  kuwa wafungwa 44  wamekutwa  wamefariki  katika  chumba walimokuwa," Tom alisema, na  kuongeza  kuwa  alifika  katika  eneo hilo.

Nigeria Soldat in gepanzertem Fahrzeug in Maiduguri
Wanajeshi wakilinda doria dhidi ya wapiganaji wa Boko HaramPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Gambrell

Chanzo cha vifo hakijajulikana

"Tumezika  miili 40  na  kupeleka  miili minne  katika  uchunguzi  wa kitabibu kwa  ajili  ya  kujua  chanzo cha  vifo  hivyo." Uchunguzi unaendelea  kubaini kile  kilichotokea  kwa  wafungwa  hao hadi wakafariki, alisema.

Duru  za  usalama, zikizungumza kwa  masharti ya  kutotajwa  jina kililiambia  shirika  la  habari  la  AFP  kuwa "wafungwa  hao 58 waliwekwa  katika  chumba  kimoja na  hawakupewa  kitu cha  kula ama  kunywa  kwa  siku  mbili".

Mahamat Nour Ahmed Ebedou, katibu  mkuu  wa  chama cha ulinzi wa  haki  za  binadamu  nchini  Chad, (CTDDH), ametoa  shutuma kama  hizo.

Nigeria Flüchtlingscamp in Maiduguri
Mamia kwa maelfu ya watu wamekimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya kundi la Boko Haram katika nchi za Afrika magharibiPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Alamba

Maafisa  wa  jela  waliwafunga  wafungwa  hao  katika  chumba kidogo na  hawakuwapa  chakula  ama  maji kwa  siku  tatu kwasababu  walikuwa  wanashutumiwa  kuwa  katika  kundi  la  Boko Haram", Ebedou aliliambia  shirika  la  habari la  AFP. "Ni unyama kile  kilichotokea."

Serikali  imekana  madai  hayo.

"Hakukuwa  na  kuwatendea  vibaya," Waziri  wa  sheria  wa  Chad , Djimet Arabi, ameliambia  shirika  la  habari  la  AFP kwa  simu.