Wapatanishi wa migogoro wakutana wabadilishane mawazo huko Zanzibar
24 Aprili 2007Matangazo
Mkutano huo unawajumuisha wapatanishi watakaoijadili changamoto zinazosababishwa na vita barani Afrika na wakati huo huo kutafuta mbinu za kusuluhisha baina ya makundi yanayozozana duniani kote.
Dr. Salim Ahmed Salim mjumbe maalum wa umoja wa nchi za Afrika na mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya amani ya Sudan kwanza anaelezea nini hasa madhumuni ya mkutano huo.