1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapatanishi wa Israel waelekea Qatar

Tatu Karema
26 Februari 2024

Maafisa wa Israel wako nchini Qatar kushughulikia mapatano ya kusimamisha vita katika Ukanda wa Gaza na makubaliano ya kuachiwa huru mateka, ambayo mshirika wake mkuu, Marekani, inasema yatafikiwa hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4cuBi
Israel | Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.Picha: Abir Sultan/AP/dpa/picture alliance

Chanzo kutoka serikali ya Israel kimesema ujumbe wake unawahusisha maafisa kutoka Shirika la Ujasusi la Mossad, ambao wamepewa jukumu la kuanzisha mkakati wa kusaidia katika majadiliano hayo.

Majukumu hayo ni pamoja na kuchuja orodha ya wapiganaji ambao kundi la Hamas linataka waachiliwe kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana mateka.

Duru za kiusalama za Misri zimesema mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana yanayohusisha wajumbe kutoka Israel na Hamas yataongozwa na wapatanishi mjini Doha, Qatar, wiki hii na baadaye mjini Cairo, Misri. 

Hata hivyo, Israel na mwenyeji Qatar hawajatoa tamko rasmi kuhusu mazungumzo hayo.