1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wapalestina kadhaa wauawa katika mashambulizi Gaza

27 Juni 2024

Watu saba wameuawa katika mashambulizi yalilofanywa na jeshi la Israel katika Jiji la Gaza, hii ikiwa ni kulingana na vikosi vya ulinzi vya Hamas vinalodhibiti eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4hbFE
Mji wa Gaza | Uharibifu baada ya mashambulizi ya Israel
Vyombo vya habari vimeripoti juu ya mashambulizi makubwa kwenye eneo la mji wa Gaza.Picha: Omar Al-Qattaa/AFP/Getty Images

Raia kadhaa wa Palestina wamejeruhiwa katika shambulizi hilo la bomu katika eneo la makaazi ya watu la Shejaiya limesema jeshi hilo, huku vyombo vya habari vikiripoti juu ya mashambulizi makubwa kwenye eneo hilo.

Jeshi la Israel limesema haliwezi kuthibitisha maafa yaliyotokana na mashambulizi hayo.

Kulingana na wizara ya afya inayoongozwa na Hamas, karibu watu 37,765 wameuawa na wengine 86,429 wamejeruhiwa huko Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita Israel kwenye Ukanda huo.