1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muungano wa utafiti wa msitu wa mvua wa Kongo wazinduliwa

3 Desemba 2023

Wanasayansi wanaohudhuria mkutano wa COP28 mjini Dubai, wamezindua muungano wa utafiti unaolenga kurekebisha ukosefu wa taarifa za kihistoria kuhusu Bonde la Mto Kongo na msitu wake wa mvua

https://p.dw.com/p/4Zj6c
Msitu wa mvua wa kitropiki wa Bonde la Kongo
Msitu wa mvua wa KongoPicha: M.Harvey/WILDLIFE/picture alliance

Jopo hilo la Sayansi ya Bonde la Mto Kongo, linalenga kutoa ripoti ifikapo mwaka 2025 ambayo itatoa tathmini ya kina zaidi ya kisayansi kuhusu Bonde la Kongo.

Mwenyekiti mwenza wa jopo hilo ambaye pia ni mtaalamu katika chuo kikuu cha Kinshasha nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Raphaël Tshimanga, amesema wanazungumzia kuhusu mfumo wa kipekee wa ikolojia ambao unawasaidia mamilioni ya watu, na pia kutekeleza jukumu muhimu katika udhibiti wa hali ya hewa ya Dunia.

Takriban wanasayansi 300 wanatarajiwa kuchangia ripoti ya Kongo

Tshimanga ameongeza kuwa uelewa wao wa sasa kuhusu utendaji kazi wa mfumo wa ikolojia wa bonde la Kongo ni mdogo mno.

Mtaalamu huyo ameongeza kuwa zaidi ya wanasayansi 300 wanatarajiwa kuchangia katika ripoti hiyo ya Kongo.