1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger: Wanajeshi 5 wafa katika shambulizi

11 Aprili 2023

Watu wenye silaha wamewaua wanajeshi watano wa jeshi la Niger waliokuwa wakiusindikiza msafara wa wachimbaji wa dhahabu katika eneo moja, kaskazini mwa nchi hiyo kunakopakana na Algeria

https://p.dw.com/p/4Pu3m
USA Soldaten aus afrikansichen Ländern bei der Militärakademie in Jacqueville
Picha: Issouf Sanogo/AFP

Duru za usalama zimeliambia shirika la habari la AFP kwamba watu hao waliojihami kwa silaha walijichanganya na msafara huo kabla ya kuwafyatulia risasi wanajeshi walioandamana na wachimbaji hao siku ya Jumapili.

Manusura mmoja wa shambulizi hilo ameliambia gazeti la mtandaoni la Air Info, lenye makao yake kwenye mji wa kaskazini mwa nchi hiyo, Agadez, wanajeshi watano pia wamejeruhiwa.

Afisa mmoja wa eneo hilo aliiambia AFP kwamba washambuliaji hao huenda walikimbia na kiasi fulani cha dhahabu na walionekana kuwa na taarifa za kutosha kuhusu msafara huo.

Mashambulizi dhidi ya wachimbaji wa dhahabu  yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika mkoa wa Agadez, ambao biashara haramu za silaha na wahamiaji kupitia eneo kubwa la jangwa nchini Niger na linalopakana na Libya na Algeria, imeshamiri.