1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wawateka nyara watu katika msikiti Kashmir India

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfkX

SRINAGAR-KASMIR:

Watu wapatao watano wanashikiliwa mateka katika msikiti mmoja na kundi la waislamu wenye msimamo mkali katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India.

Msemaji wa polisi amesema kuwa wanamgambo hao wa kundi la Hizbul Mujahideen, wamewafyatulia risasi polisi na raia wakiwa ndani ya msikiti kusini mwa eneo wilaya ya Kulgam.

Watu watatu raia wa kawaida na wengine wawili wanajeshi ndio walijeruhiwa katika risasi za mwanzo zilizofyatuliwa na wapiganaji hao.Watu watano waliokuwa wanasali katika msikiti huo baadae walichukuliwa mateka.

Eneo hilo limezingirwa na viksi vya usalama ambapo watekaji hao wanataka kujadiliana na serikali.