Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na tatizo la mikopo Tanzania
Josephat Charo Nyiro11 Mei 2016
Pamekuwa na malalamiko miongoni mwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania, kwamba pesa za mikopo zinacheleweshwa na vigezo vya kutoa mikopo vibadilishwe. Boniphace Maiga Juma, mwenyekiti wa baraza la marais wa vyuo vikuu Tanzania, anazungumzia suala hilo na DW.