1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliokufa ajali ya boti Kongo wafikia 78

4 Oktoba 2024

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mkasa wa kuzama kwa boti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefikia 78 huku juhudi za kuwatafuta wengine zinaendelea siku moja tangu mkasa huo ulipotokea.

https://p.dw.com/p/4lPFq
DR Kongo Kivu
Mmoja wa watu waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.Picha: Ruth Alonga

Gavana wa mkoa wa Kivu Kusini, Jean-Jacques Purusi, amesema idadi hiyo ya vifo ni ya awali na kuna uwezekano mkubwa ikaongezeka wakati waokoaji wanajaribu kuwatafuta wengine ambao bado hawajulikani walipo.

Soma zaidi: Watu 126 wafa maji Kongo

Amesema taarifa zinaonesha chombo hicho kilichozama kwenye Ziwa Kivu kilikuwa kimepakia abiria wasiopungua 278 kilipong´oa nanga kutoka bandari ya Minova iliyopo Kivu Kusini kuelekea mji wa Goma uliopo kwenye mkoa jirani wa Kivu Kaskazini.

Mashuhuda wanasema boti hiyo ilizima mita chache kutoka bandari ya Kituku ilipokuwa inajaribu kutia nanga na saa kadhaa baadaye waokoaji waliopoa miili ya watu 50.