1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kuondolewa nchini Mali

1 Julai 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana limepiga kura ya kuondoa haraka ujumbe wake wa kulinda amani nchini Mali, kama ilivyoamriwa na watawala wa kijeshi wa nchi hiyo wiki kadhaa zilizopita.

https://p.dw.com/p/4TIZ8
Malischer Außenminister verlangt Abzug von UN-Friedensmission
Picha: Loey Felipe/UN/dpa/picture alliance

Azimio hilo lililotayarishwa na Ufaransa na kuungwa mkono na wanachama wote 15 wa Baraza la Usalama linaamuru kuanza kuondolewa kwa vikosoi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali haraka iwezekanavyo.

Soma zaidi:Mali yaitaka MINUSMA kuondoka nchini humo mara moja

Linaelekeza zoezi la kuwaondoa kiasi askari 15,000 wa ujumbe unaofahamika kama MINUSMA lianze kutekelezwa leo Jumamosi na likamilike mwishoni mwa mwaka huu.

Watawala wa Mali, taifa hilo la Afrika Magharibi linalokabiliwa na uasi wa itikadi kali waliamuru kuondolewa kwa ujumbe wa MINUSMA baada ya kuwakaribisha wapiganaiji mamluki wa kirusi wa kundi la Wagner kusaidia kupambana na hujuma za wanamgambo wenye silaha.