1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakulima Ubelgiji kufunga njia za bandari ya Zeebrugge

30 Januari 2024

Wakulima nchini Ubelgiji waliokasirishwa na sera mpya za mazingira za Umoja wa Ulaya na uingizaji vyakula vya bei nafuu wanapanga kuzifunga barabara kuelekea bandari ya mizigo za Zeebrugge iliyo kaskazini mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4bq8V
 Brüssel, Ubelgiji | Waandamanaji waki wa mitaani
Waandamanaji wakiwa katika mitaa ya BrüsselPicha: NICOLAS MAETERLINCK/AFP

Gazeti la kila siku la De Tijd limeripoti kuwa wakulima hao wanalenga kuzuia kufukiwa bandari hiyo iliyo ya pili kwa ukubwa nchini Ubelgiji kwa muda wa saa 36 zinazokuja.

Polisi imesema imeuarifu uongozi wa bandari ya Zeebrugge kuhusu mipango hiyo ya wakulima ambao wamekusanya mamia ya matrekta na malori kwa dhima ya kuzifunga barabara.

Soma pia:Wakulima waandamana nchini Ufaransa kuishinikiza serikali itazame hatma ya sekta hiyo

Hatua hiyo itaendelea licha ya tangazo kuwa- waziri mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo anapanga kukutana na vyama vya wakulima leo Jumanne.

Maandamano hayo yanafuatia mengine yaliyofanywa na wakulima karibu kote barani Ulaya ikiwemo nchini Ujerumani, Poland, Ufaransa na Romania.