1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajuwe watuhumiwa wanne wanaotakiwa na ICC kwa vurugu za Kenya

23 Januari 2012

Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ya mjini The Hague imethibitisha mashtaka dhidi ya watuhumiwa wanne kati ya sita waliodaiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/13obI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha wa Kenya, Uhuru Kenyatta.Picha: AP

Ghasia hizo zilisababisha umwagikaji mkubwa wa damu katika taifa hilo la Afrika Mashariki ambako watu kiasi ya 1,100 waliuwawa. Kufuatia hatua ya ICC. Wakenya sasa wanasubiri kuona hatma ya mwelekeo wa hali ya mambo nchini humo. Je ni kina nani haswa wanaotakiwa mbele ya mahakama ya ICC?

Uhuru Kenyatta

Uhuru Kenyatta mwenye umri wa miaka 50 ni naibu waziri mkuu na waziri wa fedha katika serikali ya sasa ya Kenya. Ni mmoja kati ya watu wenye usemi mkubwa kabisa na pia ni miongoni mwa watu matajiri nchini humo. Jarida la Forbes lilimuorodhesha kuwa mtu wa 26 mwenye mali nyingi barani Afrika.

Uhuru alituhumiwa katika ripoti ya Tume ya Kitaifa juu ya haki za binadamu kwamba alihudhuria mikutano mapema mwaka 2008 ya kuandaa ghasia za kulipiza kisasi za jamii ya Wakikuyu kabila ambalo anatokea. Uhuru ni mwanawe rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta. Alisomea nchini Marekani na anaangaliwa kama kiongozi wa juu wa kisiasa katika kabila la Kikuyu ambalo ni kabila kubwa nchini Kenya.

Mahakama ya ICC imeridhika kwamba alihusika katika kuwaleta pamoja wanachama wa kundi haramu la kihalifu la Mungiki linalowajumuisha Wakikuyu. Kundi hilo linasadikiwa lilihusika katika kuwatahiri na kuwauwa wafuasi wa chama cha ODM.

William Samoei Ruto

William Ruto mwenye umri wa miaka 45 ni mbunge wa Eldoret Kaskazini na alikuwa kiongozi wa juu katika chama cha ODM cha waziri mkuu Raila Odinga wakati wa uchaguzi uliozua utata mwaka 2007 na kusababisha ghasia.

William Samoei Ruto
William Samoei RutoPicha: AP

Mahakama ya ICC imemtaja mwanasiasa huyo kama kiranja mkuu wa mipango ya uhalifu dhidi ya wafuasi wa chama cha Rais Mwai Kibaki cha PNU. Mwanasiasa huyo kijana na mwenye malengo makubwa ya kisiasa aliyeingia katika mvutano na kujitenga na Odinga na kutimuliwa serikalini mwaka 2010 anaangaliwa kama kiongozi wa kisiasa katika jamii ya Wakalenjin.

Ripoti nyingi zilizowahi kutolewa zimemtuhumu kwa uchochezi, kupanga na kufadhili ghasia na kikubwa zaidi anadaiwa kuwahi kutamka waziwazi kwamba watu wasiokuwa Wakalenjin katika eneo lake la bunge wanabidi kung'olewa na kuchomwa.

Ruto ni baba wa watoto sita akitokea katika familia yenye busara. Aliwahi hata kuwa mchuuzi wa karanga katika barabara za miji ya Kenya kwa ajili ya kuilisha familia yake. Ametangaza azma ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao, Marchi mwaka 2013.

Francis Kirimi Muthaura

Huyu ni afisa wa ngazi ya juu serikalini. Ana umri wa miaka 65, ni kiongozi wa utumishi wa serikali, ni katibu wa bunge na mwenyekiti wa kamati ya ushauri wa masuala ya usalama wa kitaifa. Anatajwa kuwa mtu wa karibu wa chama cha PNU cha Rais Kibaki na aliwahi kushikilia nyadhifa nyingi za kibalozi chini ya Rais Daniel Arap Moi.

A Kenyan man sits in the cab of a destroyed truck used as a makeshift roadblock while a tyre burns on the roof, as he and others enforce the roadblock in Kisumu, Kenya, Tuesday, Jan. 29, 2008. The town of Kisumu is now almost completely ethnically cleansed of Kikuyus, and mobs armed with makeshift weapons erect burning roadblocks and search for the few Kikuyu targets remaining. (AP Photo/Ben Curtis)***Zu Dohrenbusch, Keine Entspannung der Lage in Sicht - Kenianischer Oppositionspolitiker in Nairobi erschossen***
Kenia Gewalt Jugendliche brennendes AutoPicha: AP

Inaaminika kwamba alihusika katika mikutano mingi iliyofanyika katika Ikulu ya Rais ambayo ilihudhuriwa pia na Uhuru Kenyatta. Kwa mujibu wa uchunguzi uliobainishwa katika Tume ya Uchunguzi ya Waki iliyoundwa baada ya ghasia za uchaguzi. Mikutano hiyo ilitumiwa kupanga mashambulizi ya Wakikuyu ya ulipizaji kisasi katika maeneo ya miji ya Naivasha na Nakuru.

Joshua Arap Sang

Ni mtangazaji mwenye umri wa miaka 36 wa kituo cha redio cha FM kinachotangaza kwa lugha ya Kikalenjin, na ni mtuhumiwa pekee miongoni mwa sita ambaye sio afisa wa serikali na si mwasiasa.

Kenyan President Mwai Kibaki, left, and former U.N. Secretary-General Kofi Annan, center, and opposition leader Raila Odinga, right, observe a minute of silence for the victims of the recent violence, Tuesday, Jan. 29, 2008 during the opening of the "dialogue process," in Nairobi. Kibaki and Odinga together with mediator Annan formally opened the "dialogue process," with the rivals under international pressure to share power. Odinga insisted what needed "the most urgent attention" was the resolution of the flawed election results, an issue Kibaki has indicated is not negotiable.(AP Photo/Karel Prinsloo)***Zu Dohrenbusch, Keine Entspannung der Lage in Sicht - Kenianischer Oppositionspolitiker in Nairobi erschossen***
Kenia Gewalt Kofi Annan mit Mwai Kibaki und Raila OdingaPicha: AP

Mtangazaji huyo kijana ni maarufu na kipindi chake cha asubuhi kinachoitwa Lenee Emet, kwa lugha ya kiswahili ikimaanisha "Yanayotendeka nchini''. Ripoti ya Tume ya Kitaifa juu ya Haki za Binadamu ilimtuhumu mtangazaji huyu kwamba alitumia kipindi chake hicho kuwakusanya waliofanya mashambulizi na kupanga pamoja na kuchochea ghasia hizo. Aliwaita watu ambao hawakupiga kura kama walivyopiga jamii ya Wakalenjin kuwa ni wasaliti. Ameapa kutoa changamoto dhidi ya uamuzi wa ICC.

Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri:Othman Miraji