1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya kibinaadamu yazidi kuwa mbaya Gaza

25 Agosti 2024

Kundi la wanamgambo la Hamas limesema wajumbe wake wamewasili mjini Cairo, kusikiliza majadiliano ya hivi karibuni ya wapatanishi wa mgogoro huo wanaojaribu kupata makubaliano ya usitishwaji vita na kuachiwa kwa mateka.

https://p.dw.com/p/4jsxG
Ukanda wa Gaza
Wajumbe wa Hamas wako Cairo wakati hali ya kibinaadamu ikizidi kuwa mbaya GazaPicha: Jehad Alshrafi/AP/picture alliance

Hii ni baada ya Umoja wa Mataifa kuripoti hali mbaya ya kibinaadamu inayozidi kudorora huku utapia mlo ukishamiri pamoja na visa vya ugonjwa wa polio. 

Haya yanajiri wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake Gaza na kusababisha mauaji ya watu 50. Serikali imesema waathiriwa bado wapo barabarani na wengine wamenaswa chini ya vifusi vya majengo yaliyoshambuliwa. 

Marekani yasema hatua zimepigwa katika mazungumzo ya Gaza

Miezi kadhaa ya mazungumzo ya kusitisha mapigano yameshindwa kupata suluhu ya kudumu katika mgogoro huo wa Mashariki ya kati.  

Hamas inaituhumu Israel kwenda kinyume na mambo iliyokubali hapo awali jambo ambalo Israel inakanusha. Hamas imesema kuwa Marekani haina nia njema katika jukumu lake la upatanishi.