1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Wairan watoa heshima zao za kwa Raisi

21 Mei 2024

Maelfu ya Wairan wamekusanyika leo kutoa heshima zao za mwisho kwa rais Ebrahim Raisi na maafisa wengine waliofariki katika ajali ya helikopta.

https://p.dw.com/p/4g6A3
Iran Tabriz Beisetzung Präsident Raisi
Picha: Fatemeh Bahrami/Anadolu/picture alliance

Wakiwa na bendera za Iran na mabango ya picha ya rais, waombolezaji walianza safari kutembea nyuma ya lori lililobeba majeneza ya Raisi na maafisa wengine saba, kutoka kiwanja cha katikati ya mji wa Tabriz kaskazini magharibi, ambako Raisi alikuwa akielekea wakati helikopta yake ilipoanguka Jumapili iliyopita.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alitangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa na kumteua makamu wa Mohammad Mokhber kuwa rais wa mpito mpaka uchaguzi wa rais utakapofanyika Juni 28.