1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahusika wa siasa kali wafunguliwa mashtaka Uingereza

16 Agosti 2024

Polisi nchini Uingereza imewashtaki watu wawili – mwanamume mwenye umri wa miaka 18 na mwanamke mwenye umri wa miaka 19 kwa makosa ya ugaidi.

https://p.dw.com/p/4jXZm
England | Staatliche Eröffnung des Parlaments 2024 | Proteste
Picha: Vuk Valcic/ZUMA Press Wire/IMAGO

Hii ni baada ya uchunguzi wa tuhuma za kuhusika na shughuli za kigaidi zinazodaiwa kuchochewa na makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia.

Rex William Henry wa Ilford, mashariki mwa London ameshtakiwa kwa kupanga vitendo vya kigaidi wakati Sofija Vinogradova wa Cheshunt, Hertfordshire, ameshtakiwa pia kwa kupanga vitendo vya kigaidi na kukusanya habari ambazo zinaweza kumsaidia mtu kufanya vitendo vya ugaidi.

Polisi imeeleza kuwa uchunguzi wao haukuwa na uhusiano na ghasia na mashambulizi ya kibaguzi yaliyotokea Uingereza baada ya wasichana watatu kuuawa katika mji wa Southport, kaskazini mwa Uingereza.

Wawili hao wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Westminster baadaye leo.