IOM lahofia vifo vya baharini kuchukuliwa kawaida
2 Oktoba 2023Matangazo
Bi Amy Pope ameapa kufanya kazi na serikali husika kutoa njia mbadala za kiuchumi kushughulikia mgogoro uliopo wa wahamiaji.
Pope ambaye ni mshauri wa zamani wa Ikulu ya Marekani ameanza majukumu yake katika shirika hilo la IOM hii leo wakati kukiwa na mvutano wa kisiasa juu ya wahamiaji.
Amy Pope amesema ziara yake ya kwanza itakuwa katika mataifa ya Afrika Mashariki atakakokutana na wajumbe wa kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia kisha ataelekea mjini Brussels kukutana pia na maafisa wakuu wa Ulaya kujadili na kutafuta mpango wa kushughulikia uhamiaji usio wa kawaida.