1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo: Wagombea urais wataka uchaguzi huru na haki

24 Novemba 2023

Wagombea sita wa upinzani katika uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameiomba Mahakama ya Kikatiba kuishurutisha tume ya uchaguzi kuchapisha orodha ya mwisho ya wapiga kura.

https://p.dw.com/p/4ZOc5
Mkutano wa hadhara wa kisiasa wa mgombea urais Kongo Felix Tshisekedi
Wafuasi wa mgombea urais na rais wa Kongo Felix TshisekediPicha: JUSTIN MAKANGARA/REUTERS

Wagombea hao akiwemo mgombea mkuu wa upinzani Martin Fayulu na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Daktari wa Wanawake Denis Mukwege anayegombea kwa mara ya kwanza, wanadai kuwepo makosa ya makusudi yaliyofanywa na tume ya uchaguzi ambayo yanatilisha shaka uhalali wa daftari la wapiga kura. 

Soma pia:Kuondolewa vipeperushi vya wagombea kunazusha mvutano Kongo

Msemaji wa tume ya uchaguzi ya Congo - CENI amekataa kuzungumzia habari hizo.

Mkuu wa tume hiyo katika siku za nyuma alipinga tuhuma hizo, akiliambia shirika la habari la Reuters kuwa tume hiyo itahakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na wa haki.