1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagiriki wapiga kura katika uchaguzi wa bunge

21 Mei 2023

Nchini Ugiriki leo hii kunafanyika uchaguzi wa wabunge, katika mchakato unaotoa nafasi kubwa kwa chama tawala cha kihafidhina Nea Dimokratia (ND) cha Waziri Mkuu, Kyriakos Mitsotakis.

https://p.dw.com/p/4Rd61
Griechenland, Athen | Parlamentswahlen | Stimmabgabe von Kyriakos Mitsotakis
Picha: Thanassis Stavrakis/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa uchungzi wa maoni chama cha upinzani cha mrengo wa shoto cha Syriza, kikiwa na mgombea wake mkuu  waziri mkuu wa zamani Alexis Tsipras kinabashiriwa kuchukua nafasi ya pili.Kura za maoni za hivi karibuni zilionyesha chama cha Mitsotakis kitapata karibu asilimia kilifuatwa na Syriza  kwa asilimia 7.Takriban wapiga kura milioni 9.8 waliotimiza masharti ya kupiga kura wanaweza kuchagua miongoni mwa vyama 36 vilivyosajiliwa.Baada ya zoezi la kupiga kura vituo vya kupiga kura vitafungwa saa moja usiku. Na matokeo yanatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia saa mbili usiku wa leo.