1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEcuador

Ecuador: Wafungwa wawashika mateka maafisa wa magereza

1 Septemba 2023

Wafungwa katika gereza moja mjini Cuenca nchini Ecuador wanawashikilia mateka walinzi 50 wa gereza na maafisa saba wa polisi. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Juan Zapata.

https://p.dw.com/p/4VpCL
Msako wa pamoja wa jeshi na maafisa wa polisi katika gereza moja nchini Ecuador mnamo Agosti 12, 2023
Msako wa pamoja wa jeshi na maafisa wa polisi katika gereza moja nchini EcuadorPicha: Gerardo Menoscal/AFP/Getty Images

Tukio hilo limetokea siku moja baada ya mamia ya wanajeshi na maafisa wa polisi kufanya operesheni ya kutafuta silaha, risasi na vilipuzi katika moja ya magereza makuu nchini humo mjini Latacunga Kusini mwa nchi hiyo.

SNAI yasema tukio la kushika mateka ni la kisasi

Mapema, ofisi ya serikali inayosimamia magereza SNAI, ilisema kuwa hatua ya kuwashika mateka maafisa hao ni kisasi cha operesheni hiyo, lakini mamlaka baadaye ilisema hatua hiyo ilikuwa ni ya kupinga uhamisho wa wafungwa hadi magereza mengine.

Magereza ya Ecuador yamekuwa maeneo ya mauaji

Magereza ya Ecuador yamekuwa maeneo ya mauaji ya magenge hasimu yenye uhusiano na magenge ya Colombia na Mexico ambayo yamesababisha vifo vya wafungwa zaidi ya 430 tangu 2021.