1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa rais wa zamani na wa sasa wapambana Bolivia

23 Septemba 2024

Wafuasi wa serikali na maafisa wa usalama wa Bolivia wamepambana na waandamanaji wanaomuunga mkono rais wa zamani, Evo Morales, kwenye mitaa ya mji wa El Alto, ikiwa ni mara ya pili kwa tukio kama hilo kutokea wiki hii.

https://p.dw.com/p/4kxRT
Wafuasi wa Evo Morales wakikabiliana na waungaji mkono wa serikali ya Bolivia.
Wafuasi wa Evo Morales wakikabiliana na waungaji mkono wa serikali ya Bolivia.Picha: Juan Karita/AP/picture alliance

Waandamanaji hao walirushiana mawe na mabomu ya kienyeji hapo jana,  huku polisi wakiwapuliza gesi ya machozi. Watu wanane wamejeruhiwa, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Bolivia.

Makabiliano hayo yametokea wakati maelfu ya wafuasi wa Morales wakiendelea na safari yao ya kilomita 190 wiki nzima kuelekea mji mkuu, La Paz, kupinga siasa za uhasama wakati taifa hilo la Andean likielekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani.

Soma zaidi: Rais Luis Arce wa Bolivia amtuhumu kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Evo Marales kwa kupanga njama ya mapinduzi

Morales na aliyekuwa waziri wake wa uchumi na kugeuka hasimu wake, rais wa sasa Luis Arce, wanawania kukiongoza chama tawala cha kisoshalisti, MAS, kuelekea mwaka 2025.