1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachungaji wanaotuhumiwa na mauaji kufikishwa mahakamani

2 Mei 2023

Wachungaji wawili nchini Kenya wamefikishwa mahakamani leo kwa kushukiwa kuhusika na vifo vya kiasi watu 109 waliokutwa wamezikwa katika kile kinachoitwa mauaji ya watu wengi ya msitu wa Shakahola, kaunti ya Kilifi.

https://p.dw.com/p/4QnJP
Polizisten eskortieren Ezekiel Ombok Odero im Polizeipräsidium in Mombasa
Picha: Stringer/REUTERS

Paul Nthenge Mackenzie aliyejitangaza kuwa mchungaji na kuunda kanisa lake linaloitwa Good News International mwaka 2003 anatuhumiwa kuwachochea wafuasi wake kuishi bila ya kula wala kunywa chochote mpaka wafe na kukutana na Yesu, alifikishwa mahakama ya Malindi kujibu kesi.

Jamaa na familia za wahanga walimiminika ndani ya chumba kidogo cha  mahakama hiyo, Mackenzie akisindikizwa na maafisa kadhaa wa polisi akiwa pamoja na watuhumiwa wengine wanane.

Waendesha mashtaka mjini Mombasa wanataka Mchungaji mwingine maarufu Ezekiel Odero ambaye ana utajiri mkubwa nchini humo azuiliwe kwa siku nyingine 30 zaidi.

Mchungaji huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Mombasa, baada ya kukamatwa alhamisi wiki iliyopita, akituhumiwa kuhusika miongoni mwa mengine, kusaidia mauaji, utekaji nyara, kuchochea itikadi kali za kidinina uhalifu dhidi ya ubinadamu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW