1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPeru

Wabunge wa Peru wawasilisha ombi la kumng'oa rais Boluarte

26 Januari 2023

Wabunge kadhaa nchini Peru wamewasilisha hoja ya kumuondoa madarakani rais Dina Boluarte.

https://p.dw.com/p/4MicN
Rais wa Peru, Dina Boluarte
Rais wa Peru, Dina BoluartePicha: Angela Ponce/REUTERS

Wabunge 28 wa mrengo wa kushoto na wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani mwishoni mwa mwaka uliopita Pedro Castillo wamesaini hati ya ombi hilo, lililohitaji kuanzia saini 26 ili kuwasilishwa.

Ombi hilo kwa sasa linahitaji kuidhinishwa kwa kura 52 kabla ya kujadiliwa bungeni, ambako litahitaji kupigiwa kura na theluthi mbili ya wabunge.

Sehemu ya ombi hilo inasema haijawahi kushuhudiwa nchini Peru kwa serikali iliyotawala kwa muda mfupi kuwaua watu zaidi ya 40 walioandamana, na kumtuhumu rais Boluarte kutumia nguvu kubwa, miongoni mwa madai mengine.

Ofisi ya rais Boluarte hata hivyo haikuwa tayari kuzungumzia hilo ilipooombwa kufanya hivyo.