1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Kenya kupiga kura ya kumuondoa au la Gachagua

8 Oktoba 2024

Wabunge nchini Kenya wanatarajiwa hivi leo jioni kupiga kura ya kuamua iwapo wanamuondoa madarakani au la naibu wa rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua.

https://p.dw.com/p/4lWzt
Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua
Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua akitoa hotuba yake wakati wa ibada ya kumbukumbu ya waathiriwa wa moto huko Mweiga Septemba 26, 2024.Picha: LUIS TATO/AFP

Gachagua, ambaye atapata fursa ya kujitetea mbele ya wabunge, alisema hapo jana kuwa hatojiuzulu nafasi hiyo huku akikanusha tuhuma zote zinazomkabili, ikiwa ni pamoja na kujilimbikizia mali kinyume cha sheria, kuihujumu serikali na kutoa matamshi ya kuchochea ukabila. Kiongozi huyo amekuwa akiandamwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na hata wananchi wanaomtaka ajiuzulu. Usalama umeimarishwa jijini Nairobi kwenye maeneo ya bunge wakati Gachagua akisubiri kujua hatima yake hii leo.